Jumamosi, 10 Agosti 2013

Wivu nouma! Demu achoma Range Rover Sport kisha kondomu aliyoikuta katika gari la boyfriend wake

WIVU ukizidi huwa ni noma sana! Mdada mmoja mkazi wa Mbezi amelitia kiberiti na kuliuguza gari la mpenzi wake aina ya Range Rover Jipyaaa kabisa kwa kile kilichoelezwa wivu wa mapenzi.
Inadaiwa kuwa mwanadada huyo aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kukuta mpira wa kiume (condom) iliyotumika ndani ya  gari hilo kuashiria kuna mwenzake kamong'nyolewa punde. Mashuhuda wa tukio hilo wanatonya kuwa wakati analiwasha moto alikuwa akisema kuwa hili gari ndilo linakutia kiburi mpaka kutembea na wanawake zako ndani ya gari, tuone sasa ukitaka katembee nao vichakani....!