Jumatatu, 1 Julai 2013

Shirika la Ndege kuajiri wanawake tu, kisa....!

Mmoja wa wahudumu wa kike kwenye ndege hiyo.
Shirika moja la ndege za gharama nafuu nchini India limeamua kuajiri wahudumu wa kike pekee kuokoa fedha kwenye bili yake ya mafuta.
GoAir limesema kwamba kubeba wahudumu wa kike pekee kutaokoa Rupia milioni 30 (Pauni za Uingereza 330,000) kwa mwaka sababu wana uzito wa kati ya 33lb hadi 44lb pungufu ya wastani kuliko wenzao wa kiume.
Wafanyakazi 132 wa kiume kwenye shirika hilo hawatafukuzwa sababu hakutakuwa na nyongeza katika vyeo vyao.
GoAir linapanga kuongeza ndege 80 kwenye njia zake kuu 15 hadi kufikia mwaka 2020, limeripoti gazeti la Times of India, na litaajiri wahudumu 2,000 wa kwenye ndege na marubani.
Pia litapunguza ukubwa wa jarida lake la kwenye ndege na kujaza matanki yake ya maji asilimia 60 tu ya uwezo wake kujaribu kuzifanya ndege zake ziwe na uzito mdogo.
Kampuni hiyo inakadiria kwamba kila kilo ya uzito inaligharimu shirika hilo Rupia 1.7 kwa saa moja angani.
Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Giorgio De Roni ameishutumu sarafu ya India, ambayo imeshuka thamani asilimia 27 dhidi ya Dola ya Marekani katika mwaka uliopita, kwa mahitaji hayo ya kupunguza gharama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni