Jumapili, 14 Julai 2013

Hawa ndiyo waliofanikisha Masogange na mwenzake kupelekwa 'Unga' Bondeni



HAKUNA sababu ya kumkamata ‘mchawi’  kwenye skendo ya Video Queen wa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ kudaiwa kukamatwa na madawa ya  kulevya nchini Afrika Kusini wakati ukweli upo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Watu mbalimbali ambao wamesoma sakata hili kwenye vyombo vya habari, walitoa maoni yao wakisema kuwa watu wanaotakiwa kuwajibishwa ni waliokuwa uwanjani hapo siku Masogange aliposafiri na kuruhusu mizigo ya mrembo huyo na mdogo wake, Melisa Edward ipite bila ukaguzi makini.

“Kuna uwezekano kabisa wa kuwajua watu hao,” alisema msomaji wetu, Mbande Kinaka, mkazi wa Kariakoo, Dar.
Risasi Jumamosi lilimtafuta Mkuu Kitengo cha Kudhibiti Madawa ya Kulevya Tanzania, Kamanda Godfrey Nzowa, alipopatikana na kuulizwa namna ya kuwabaini waliomruhusu Masogange akapenya na mzigo airport, alisema lazima watawapata.


Taarifa tulizozipata zinasema Agnes na mdogo wake Melisa Edward  waliondoka nchini Julai 5, mwaka huu kwenda Afrika Kusini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni