Jumapili, 28 Julai 2013

Mbunge wa CCM katika kashfa nzito ya biashara ya dawa za kulevya


HAKUNA ubishi kwamba biashara ya madawa ya kulevya mara nyingi hubebwa na hufanywa na watu wenye nazo au wenye madaraka fulani makubwa. Ni biashara ambayo ina faida kubwa na ya haraka pengine kupita aina nyingine yeyote ya biashara (halali na haramu). 
Na kutokana na nguvu ya vyombo mbalimbali vya dola ulimwenguni katika kupambana na biashara hii, ni wazi kwamba bila kuwepo na connection za hali ya juu, utekelezaji wa biashara hii ungekuwa mgumu sana…
Ndio maana vita dhidi ya biashara hii haramu ni ngumu na ambayo inahitaji umakini wa hali ya juu zaidi katika kukabiliana nayo endapo kuna nia ya dhati ya kuitokomeza au japo kuipunguza. 
Hivyo basi haishangazi sana (japokuwa hizi ni tuhuma tu) kusikia yale yaliyotajwa katika “barua kutoka Hong Kong” kwa miongoni mwa watanzania wanaosemekana kufikia hata 200 wanaosota katika jela za nchini humo  kusikia majina ya watu waliotajwa katika waraka huo ambao bila shaka utapamba vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania wiki kadhaa zijazo. 
Kutajwa kwa wazi wazi kwa majina ya baadhi ya wanaotuhumiwa kuhusika na huku mwandishi wa barua hiyo akionya kwamba majina mengine zaidi yapo, kunaifanya barua hiyo kuwa tofauti kabisa na barua za kawaida au hata zile tambo za kisiasa kwamba “wanaohusika na biashara hii nawajua” 
Miongoni mwa majina hayo, limo jina la Mbunge wa Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Idd Mohammed Azan. 
Barua hiyo (ambayo utaisoma hapa chini) inahitaji kufanyiwa uchunguzi wa kina. Lakini kutokana na ukweli kwamba imeainisha watu wanaosadikiwa kuhusika, bila shaka imelipa jeshi la polisi mahali pazuri pa kuanzia. Je,wanaotajwa kipato chao kinatokana na biashara gani zilizo halali? Ukaguzi wa vitabu vyao vya fedha unasemaje? 
Jambo moja ambalo linasikitisha sana (endapo tuhuma hizi zitathibitishwa hususani kumhusu Iddi Azan) ni kwamba Jimbo au Wilaya ya Kinondoni ni miongoni mwa maeneo ambayo yanaongoza kwa vijana kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya. Je,ina maana Mbunge wake anahusika katika kuangamiza vijana au wapiga kura wa jimbo lake mwenyewe?

SOMA BARUA YENYEWE HAPA CHINI… baruamadawa(01)
baruamadawa(02)
baruamadawa(03)
baruamadawa(04)
baruamadawa(05)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni